Wanamapambano wa Palestina
wametungua ndege ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel iliyokuwa
inafanya mauaji dhidi ya wananchi wa Palestina.
Televisheni ya al Quds imezinukuu
Brigedi za Izuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya
Palestina HAMAS zikisema kuwa, ndege za utawala wa Kizayuni zimefanya
mashambulizi makali katika eneo ilipoanguka ndege hiyo ya Israel ili
kufuta ushahidi na kuwazuia wanamapambano wa Palestina wasipate mabaki
ya ndege hiyo.
Vile vile wanamapambano wa Palestina
wamefanikiwa kwa mara ya kwanza kushambulia maeneo ya Wazayuni katika
mji wa Baytul Muqaddas na kuzusha kiwewe katika safu za utawala wa
Kizayuni.
Kabla ya hapo pia HAMAS ilikuwa
imetungua ndege ya Israel isiyo na rubani na ilishambulia pia Tel Aviv
mji mkuu wa utawala wa Kizayuni na kuwalazimisha viongozi wa Israel
wakimbilie mafichoni.
Televisheni ya al Quds imetangaza pia
kuwa wanapambanao wa Palestina wamelishambulia kwa kombora bunge la
utawala wa Kizayuni, Knesset, huko magharibi mwa Baytul Muqaddas.
Taarifa zinasema pia kuwa hoteli za kitalii za Wazayuni zimefungwa huko
Baytul Muqaddas baada ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni ya
mji huo kushambuliwa kwa makombora ya wanamapambano wa Palestina.


0 comments:
Post a Comment