Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday, 4 November 2012

Maalim Seif akemea kunyanyaswa Wazanzibari

Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ameelezea kuchukizwa na vitendo vya unyanyasaji wa raia wasio na hatia vilivyofanywa na Jeshi la Polisi likishirikiana na vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). Maalim Seif Sharif Hamad ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF amevilaumu vyombo vya dola kwa kutochukua hatua stahiki kudhibiti vitendo hivyo. Maalim Seif amesisitiza kwamba, hatua zilizochukuliwa katika kurejesha amani baada ya kutokea kwa vurugu hazikuwa sahihi, kwani zimekuwa zikiwadhalilisha na kuwanyanyasa wananchi wasiokuwa na hatia pamoja na kuhujumu mali zao. Katibu Mkuu huyo wa CUF ameeleza kuchukizwa pia na tukio la kuuawa kwa askari polisi, Koplo Said Abdulrahmani, katika eneo la Bububu na kuongeza kuwa, kuwa bado serikali na vyombo vya dola vina jukumu la kulinda haki za raia kwa kuwasaka waliohusika na tukio hilo badala ya kuwanyanyasa raia wasiokuwa na hatia. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ametahadharisha kuwa, huenda vitendo hivyo vimepangwa kuvuruga umoja wa Wazanzibari na kuwataka wananchi kutokubali kuingizwa katika mtego huo.

0 comments:

Post a Comment