Sikiliza Live
Sunday, 4 November 2012
UN yaonya kushambuliwa kijeshi nchi ya Mali
Umoja wa Mataifa umeonya kuhusiana na matokeo mabaya ya mashambulio ya
kijeshi ya nchi za Magharibi dhidi ya Mali. Ripoti ya Umoja wa Mataifa
imebainisha kwamba, endapo madola ya Magharibi yataishambulia kijeshi
Mali, zaidi ya watu khamsini na tano elfu wa kaskazini mwa nchi hiyo
watakuwa wakimbizi. Kufuatia kushuhudiwa hali ya mchafukoge kaskazini
mwa Mali, madola ya Magharibi ikiwemo Marekani na Ufaransa yametoa
pendekezo la uingiliaji wa kijeshi katika nchi hiyo, ilhali baadhi ya
nchi za eneo ikiwemo Algeria zinapinga pendekezo hilo. Umoja wa Mataifa
umesema kuwa, katika kipindi cha miezi saba ya ukosefu wa amani katika
nchi hiyo kutokana na harakati za waasi, watu wapatao lakini tatu wa
kaskazini mwa Mali wamekimbilia katika nchi za Niger na Algeria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
Post a Comment