Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday, 11 November 2012

Kuanza kazi mitambo ya nyuklia ya Bushehr - Iran

Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia wa Jamhuri  ya Iran amesema kuwa, katika kipindi cha miezi michache ijayo, zitafunguliwa rasmi shughuli za awali za mitambo ya nyuklia huko Bushehr kusini mwa Iran. Fereydun Abbasi ameongeza kuwa, mitambo ya nyuklia ya Bushehr itafunguliwa mwezi Januari au Februari mwakani na wataalamu wa Kiirani baada ya kufanyika majaribio kadhaa ya kitaalamu. Ameongeza kuwa, shughuli za wakandarasi wa Kirussia zinafikia ukingoni na limebakia suala la kukabidhiwa rasmi wataalamu wa Kiirani kuiendesha mitambo hiyo. Abbasi ameongeza kuwa, hivi sasa mitambo ya Bushehr ina uwezo wa kuzalisha megawati elfu moja za umeme, na kisha kiwango hicho kitaongezwa kufikia megawati elfu nne hadi  sita na hatimaye kuingizwa kwenye gridi ya taifa.

0 comments:

Post a Comment