Sikiliza Live
Sunday, 11 November 2012
Kuna udharura wa kuingilia kijeshi Mali
Rais wa Nigeria amesema kuwa, ni jambo lenye udharura kutumiwa njia ya
kijeshi huko kaskazini mwa Mali. Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria
amesema mwanzoni mwa kikao cha wakuu wa Kiafrika huko Abuja kuwa
uingiliaji wa kijeshi kwa ajili ya kuwafukuzia mbali wapiganaji wa
Kiislamu wenye misimamo mikali huko kaskazini mwa Mali na kuzuia
taathira zake kuenea katika nchi za Kiafrika ni jambo lenye udharura.
Rais wa Nigeria amesema mwanzoni kwa kikao hicho cha dharura cha wakuu
wa nchi za Kiafrika huko Abuja kuwa Nigeria itaidhinisha kikamilifu
mapendekezo ya Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Kiafrika kwa ajili
ya kutuma haraka vikosi vya wanajeshi huko kaskazini mwa Mali ili
kurejesha amani na uthabiti katika eneo hilo. Rais wa Nigeria
amesisitiza pia kuwa uingiliaji huo wa kijeshi utategemea azimio la
Umoja wa Mataifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
Post a Comment