Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday, 19 October 2012

Wamali waandamana kupinga uingiliaji wa kijeshi

Wananchi wa Mali wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Bamako wakilaani azimio la hivi karibuni la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu uwezekano wa kuingilia kijeshi mgogoro wa nchi hiyo.
Maelfu ya Wamali walijitokeza mitaani katika maandamano huku wakiwa wamebebea mabango yasemayo: ‘Hatutaruhusu kutekwa haki yetu ya kujitawala.’ Siku chache zilizopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio ambalo lilizitaka nchi za Afrika Magharibi kuwasilisha mpango wa kuingilia kijeshi mgogoro wa Mali.
Ikumbukwe kuwa baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini Mali mwezi Machi, makundi ya waasi yalichukua udhibiti wa eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Habari zaidi kutoka Mali zinasema waasi wenye misimamo mikali ya kidini wameharibu maeneo ya ziara ya Waislamu wenye itikadi za Kisufi karibu na mji wa Timbuktu kaskazini mwa nchi hiyo.

0 comments:

Post a Comment