Serikali ya Saudi Arabia imesema Waislamu wa Uganda na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu
kutokana na kuibuka ugonjwa wa Ebola katika nchi hizo mbili za Afrika.
Kiongozi wa Jamii ya Waislamu Congo Sheikh Abdalla Mangala ameelezea masikitiko yake kuwa Waislamu wa nchi hizo hawataweza kushiriki katika ibada ya Hija.
Tokea mwezi Agosti mwaka huu watu 74 wamepatikana na ugonjwa wa Ebola nchini Congo ambapo nusu yao wameaga dunia. Nchini Uganda watu 17 wamepoteza maisha tokea mwezi Julai baada ya kuambukizwa ugonjwa huo.
Wakati huo huo duru kutoka Saudi Arabia zinasema zaidi ya mahujaji milioni moja tayari wameshawasili nchini humo.

0 comments:
Post a Comment