Rais Barack
Obama wa Marekani ambaye ameanza safari yake ya kulitembelea bara la Afrika leo
amekutana na mwenzake wa Senegal Macky Sall.
Katika mazungumzo hayo Obama
amesifia hatua alizozitaja kuwa za kushangaza za kuimarisha demokrasia
zilizopigwa na nchi za bara la Afrika.
Ameongeza kuwa, Senegal ni moja ya
waitifaki wenye nguvu zaidi wa Marekani barani humo na kwamba nchi hiyo
inaelekea kuwa mfano mzuri wa utawala bora.
Hii ni safari ya 3 ya Obama barani
Afrika ambako atazitembelea pia nchi za Afrika Kusini na Tanzania.
Obama
amesema kuwa, ijapokuwa hali ya Mandela si nzuri lakini hatovunja safari yake
ya Afrika Kusini na kuongeza kwamba lolote lile litakalotokea Mandela
ataendelea kukumbukwa kama shujaa kutokana na mema aliyoyafanya. Katika ziara
yake hiyo nchini Senegal pamoja na mambo mengine Obama na mkewe wanatarajiwa
kutembelea kisiwa cha Goree, ambacho kilikuwa kituo cha kusafirishia watumbwa
katika pwani ya mji mkuu Dakar.
0 comments:
Post a Comment