Mapigano ya
kikabila yaliyozuka kaskazini mwa jimbo la Darfur, Sudan, yamepelekea watu 61
kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Mapigano hayo yalizuka jana yakiyahusisha
makabila mawili ya Bani Hussein na Illa Balah katika eneo la al-Sarif kaskazini
mwa jimbo hilo na kupelekea watu 39 kuuawa na wengine 22 kujeruhiwa.
Katika mapigano
hayo watu wengine kadhaa wametoweka.
Kiongozi wa baraza lililoundwa hivi
karibuni kwa minajili ya kukabiliana na migogoro ya eneo la mji huo ‘al-Sarif’
Bwana Ahmad Mahdi Hamid, ameitaka serikali ya Khartoum kufanya juhudi zaidi za
kumaliza mapigano kati ya makabila hayo mawili na kusisitizia udharura wa
kunyang’anywa silaha wanamgambo wa makabila hayo. Amesema silaha hizo zimekuwa
sababu kubwa ya kuyaingiza makabila kadhaa nchini humo katika mapigano ya
wenyewe kwa wenyewe.
Hivi karibuni Rais Omar Hasan al Bashir wa Sudan alionya
juu ya hatari ya mapigano ya kikabila ambayo yamekuwa yakitokea katika baadhi
ya maeneo ya nchi hiyo na kuyataja kuwa ni hatari kwa usalama wa taifa. Al
Bashir alisema hayo katika kikao cha Baraza la Ushauri la Kongresi ya Taifa na
kuongeza kuwa, serikali yake inakabiliwa na changamoto kubwa katika kuzuia hali
hiyo.
Wakati huo huo taarifa zinaeleza kuwa, serikali ya Sudan, imeanza tena
kusafirisha mafuta ya Sudan Kusini kupitia mabomba na bandari zake za
usafirishaji mafuta.
0 comments:
Post a Comment