skip to main |
skip to sidebar
Hollande kupambana na chuki dhidi ya Uislamu
Rais Francois Hollande wa Ufaransa ameahidi
kupambana na vitendo vya uadui na chuki dhidi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu
nchini humo. Akizungumza mbele ya mjumuiko mkubwa wa wawakilishi wa taasisi na
asasi za kiserikali na kiraia pambizoni mwa Paris, Rais Hollande amesisitiza
kuwa, vitendo vya chuki na ubaguzi hasa dhidi ya Waislamu vinapaswa kukomeshwa.
Miongoni mwa vitendo vya chuki na uadui dhidi
ya wafuasi wa dini ya Kiislamu mwaka huu, ni mashambulizi kadhaa yaliyofanywa
dhidi ya wanawake waliovaa hijabu ya Kiislamu katika eneo la Val- d'Oise
kaskazini mwa Ufaransa. Viongozi wa Muungano wa Taasisi za Kiislamu nchini
Ufaransa UOIF wamesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba, chuki na
uadui dhidi ya Waislamu limekuwa jambo la kawaida nchini humo na wamewataka
viongozi wa serikali ya Paris kuvunja kimya chao na badala yake kukabiliana na
vitendo hivyo viovu.
Nalo Baraza la Utamaduni la Waislamu nchini
Ufaransa CFCM limetangaza kuwa, zaidi ya Misikiti 10 imeshavunjiwa heshima
tokea kuanza mwaka huu wa 2013.
0 comments:
Post a Comment