Mkuu wa vikosi vya majeshi ya Libya
ameituhumu baadhi ya mirengo iliyoko kwenye bunge la nchi hiyo kwa kufanya
njama za kuzorotesha mwenendo wa kulijenga upya jeshi la nchi hiyo.
Akizungumza kwenye ukumbi wa bunge la
Libya, Meja Jenerali Salim al Gnaidy ameituhumu pia serikali ya Tripoli kwa
kuingilia masuala ya jeshi na kutoa amri na maamuzi ya kijeshi bila ya kufanya
mawasiliano yoyote na viongozi wa ngazi za juu wa jeshi. Meja Jenerali al
Gnaidy ameongeza kuwa, kuna ulazima wa kutengwa bajeti ya kutosha kwa lengo la
kulikarabati jeshi la nchi hiyo na ameikosoa mirengo inayofanya njama za kutaka
bajeti ya jeshi ipunguzwe.Baada ya kuangushwa utawala wa Kanali Muammar Gaddafi, kiongozi wa zamani wa Libya, serikali ya nchi hiyo imekuwa ikifanya juhudi za kulijenga upya jeshi la nchi hiyo na kulipatia zana na silaha za kisasa.
0 comments:
Post a Comment