Waziri wa
Mambo ya Nje wa Ethiopia ametaka yafanyike mazungumzo kati ya nchi yake na
Misri juu ya tofauti za ujenzi wa bwawa la Renaissance. Tedros Adhanom
Ghebreyesus ameyasema hayo katika kikao cha pamoja na waandishi wa habari kati
yake na Murad Mudallis waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Algeria na kuongeza
kuwa, nchi yake inataka kumaliza baadhi ya tofauti zilizosalia kuhusiana na
kadhia hiyo. Aidha Ghebreyesus ameongeza kuwa, hivi karibuni atafanya safari nchini
Misri kuitikia wito wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo Mohamed Kamel
Amr kuhusiana na kadhia hiyo. Hatua ya Ethiopia ya kutaka kujenga bwawa la
Renaissance katika mto Nile, ilikabiliwa na radiamali kali ya srikali ya Cairo
na kuibua suutafahumu kati ya nchi mbili hizo. Misri inaitaka serikali ya Addis
Ababa kufungamana na mkataba wa zamani kuhusiana na utumiaji wa maji ya mto
huo, mkataba ambao unaipa zaidi Misri na Sudan haki ya kustafidi na maji ya mto
huo, suala linalopingwa na Ethiopia inayosisitiza juu ya mkataba wa
Entebbe, Uganda unaozipa haki sawa nchi zote zinazochangia maji ya mto huo.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment