Msemaji wa
Rais Muhammad Mursi wa Misri amesema kuwa, mazungumzo ndiyo njia pekee ya
kuiepusha nchi hiyo na mgogoro wa kisiasa. Ehab Fahmy amefafanua kuwa, ikulu ya
rais imejiandaa kufanya mazungumzo ya kitaifa na ya kweli. Aidha Ehab amewataka
wapinzani kufanya maandamano ya amani. Kwa upande mwingine msemaji huyo wa rais
ametangaza kuwa, Rais Muhammad Mursi amekiri kufanya baadhi ya makosa na
kuahidi kuyarekebisha. Rais Mursi amenukuliwa akisema kuwa, Misri haitoshuhudia
mapinduzi mengine wala uchaguzi wa mapema. Mursi ameyasema hayo, alipokuwa
akiongea na mwandishi wa habari wa gazeti la The Guardian na kuwataka wapinzani
wake, kuacha maandamano. Hii ni katika hali ambayo mamilioni ya Wamisri wenye
hasira wanaendelea kufanya maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali ya nchi
hiyo wakimtaka Rais Muhammad Morsi ajiuzulu na kuitisha uchaguzi wa kabla ya
wakati. Katika upande mwingine, maelfu ya wafuasi wa Morsi nao wameandamana
wakimtaka rais huyo aendelee kusalia madarakani kwa hoja kuwa amechaguliwa kihalali
na wananchi.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment