Mbunge wa chama cha upinzani cha Republicans nchini Marekani amedai 
kwamba serikali ya nchi hiyo ndiyo iliyopanga mashambulizi ya mabomu 
huko Boston wakati wa mashindano ya mbio za masafa marefu maarufu kama 
Boston Marathon. Stella Tremblay, amesema taarifa ya serikali kuhusu 
jinsi mashambulizi hayo yalivyotokea haina muwala wala mtiririko na kwa 
mantiki hiyo inaweza kutiliwa shaka. Amesema kuna ushahidi unaoonyesha 
kuwa mabomu hayo yalitegwa na serikali ili kufikia malengo yake haramu. 
Hata hivyo, mbunge huyo wa New Hampshire hakufafanua kuhusu ushahidi 
huo. Amesema Marekani imekuwa ikitumia ndege zisizo na rubani kuwaua 
watu wasio na hatia na kana kwamba haijatosheka, sasa imeamua kumwaga 
damu za Wamarekani ndani ya nchi yao. Serikali ya Washington haijasema 
lolote kuhusu tuhuma hizo. 
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment