Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 4 April 2013

Safari ya Hollande Morocco yagubikwa na kashfa

                           23,Jumaadal ula,1434Hijiriyah/ April 04,2013Miyladiyah
 
Rais Francois Hollande wa Ufaransa ameitembela Morocco kwa minajili ya kuimarisha uhusiano na nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika koloni lake la zamani, huku wimbi la ufisadi wa mmoja kati ya mawaziri wa serikali yake likizusha gumzo kubwa nchini. Hollande amelakiwa na Mfalme Muhammad VI baada ya kuwasili mjini Casablanca ambapo amefuatana na wafanyabiashara 60 na mawaziri wasiopungua 8 na anatarajiwa leo kuhutubia Bunge la Morocco.
Safari yake hiyo ya siku mbili nchini Morocco imeathiriwa na sakata la kukwepa kodi linalomkabiliwa waziri wa bajeti wa zamani wa Ufaransa. Jerome Cahuzac amekiri kuwa alikwepa kulipa kodi ya fedha alizozificha kwenye akaunti yake ya nje kwa muda wa miaka 20.  Rais wa Ufaransa kabla ya kuelekea Morocco aliahidi kuwa atakabiliana vilivyo na wanasiasa mafisadi nchini kwake.

0 comments:

Post a Comment