Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Wednesday, 9 January 2013

Viongozi wa Hamas na Fat'h wakutana Misri

Viongozi wa harakati za Hamas na Fat-h za Palestina wamekutana nchini Misri na kufanya mazungumzo yenye lengo la kudumisha umoja miongoni mwao.
Khaled Mash'al Kiongozi wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Hamas na Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina walifanya mazungumzo katika mji mkuu Cairo hapo jana. Kabla ya hapo Rais Muhammad Mursi wa Misri alikutana na wawili hao katika vipindi tofauti.  Tarehe 4 Januari Mahmoud Abbas alitoa wito kwa harakati hizo mbili kumaliza mivutano yao ya muda mrefu na kuungana. Maafisa wa pande hizo mbili wamesema mazungumzo hayo yatajadili namna ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa, ambayo itaandaa njia ya kufanyika uchaguzi wa Bunge na Rais wa Palestina.

0 comments:

Post a Comment