Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday, 14 October 2012

'Wachezaji Waislamu Newcastle wasivae jezi za timu yao'

Wachezaji Waislamu wa timu ya Soka ya Newcastle United katika Ligi ya Premier huko England wameonywa kuwa kuvaa jezi zenye nembo ya mfadhili mpya wa timu hiyo ni ukiukaji wa sheria za Kiislamu.
Newcastle imetangaza mkataba wa Pauni £ Milioni 24 na shirika lenye utata la kutoa mikopo lijulikanalo kwa jila la Wonga. Sheikh Ibrahim Mogra Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Uingereza amesema kuwa, shirika la Wonga linawakandamiza sana watu masikini kwa kuwatoza kiasi kikubwa cha riba kwa mikopo ya muda mfupi. Wachezaji Waislamu katika timu ya Newcastle ambao ni Demba Ba, Papiss Cisse, Cheick Tiote na Hatem Ben Arfa wametakiwa watangaze msimamo wao kuhusu suala hili.

0 comments:

Post a Comment