Tunapenda
kuwakumbusha ndugu zetu wengi jambo ambalo wanaghafilika nalo, kuwa,
wenye kunuia kuchinja au kuchinjiwa, kuanzia unapoingia tu mwezi wa
Dhul-Hijjah wanatakiwa wajizuie kukata nywele na kucha mpaka
watakapomaliza kuchinja. Haya ni maamrisho yanayopatikana katika Hadiyth
ifuatayo:
عن
أم سلمة رضي الله عنها، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إذا رأيتم
هلال ذي الحجة وأراد أحدكـم أن يضحّي فليمسك عــن شعره وأظفاره) وفي راوية: ((فلا يأخذ من شعره ولا من أظفـاره حتى يضحّي)) مسلم
Imetoka kwa Ummu Salamah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukiandama mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake)
Na katika riwaya nyingine ((Asikate nywele wala kucha mpaka akimaliza kuchinja)) [Muslim na wengineo].


0 comments:
Post a Comment