Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday, 21 October 2012

Meli ya misaada ya Estelle yashambuliwa na Israel

Katibu Mkuu wa Kamati ya Ubunifu wa Taifa la Palestina amesema kuwa vikosi vya majini vya Israel vimekiuka wazi sheria za kimataifa kwa kushambulia meli ya misaada ya kibinadamu ya Estelle katika maji ya kimataifa. Mustapha Barghuthi ameongeza kuwa, shambulio hilo linaonyesha pia kushindwa na kugonga ukuta Baraza la Mawaziri la Benjamin Netanyahu ambalo linaendeleza hatua mbalimbali za jinai. Baraghuthi pia amesema kuingia meli ya Estelle katika maji ya kimataifa kunaonyesha kufanikiwa juhudi zake za kuvunja mzingiro wa Gaza na kwamba meli hiyo haijakiuka sheria yoyote ya kimataifa. Pia amezitaka nchi zote duniani kulaani hatua hiyo ya uharamia wa baharini na kuifikisha Israel katika vyombo vya sheria. Juzi vikosi vya majini vya Israel vilishambulia meli ya misaada ya kibinaadamu iliyotokea Ulaya ambayo ilikuwa imebeba misaada na wanaharakati mbalimbali wa haki za binadamu kutoka nchi 30 duniani, na kuizuia kutia nanga katika Ukanda wa Gaza. Meli hiyo imepeleka katika bandari inayodhibitiwa na Israel ya Ashdod.

0 comments:

Post a Comment