Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday, 21 October 2012

Khamis Gaddafi auawa katika mapigano Libya

Serikali ya Libya imetangaza kuwa Khamis Gaddafi mwana mdogo wa Muammar Gaddafi ameuawa katika mapigano makali yaliyojiri katika mji wa Bani Walid.
Naibu Waziri Mkuu wa Libya Mustafa Abu Shagur amethibitisha habari za kuuawa Khamis Gaddafi na kusema mwili wake uko katika hospitali ya Misrata kaskazini mashariki mwa Bani Walid.
Khamis ambaye ni mwana wa saba na mdogo zaidi wa dikteta Gaddafi ameuawa baada ya vikosi vya serikali kuuzingira mji wa Bani Walid kwa lengo la kuwatimua wanamgambo watiifu kwa dikteta aliyeuawa Muammar Gaddafi.
Imearifiwa kuwa watu wengine 26 wameuawa katika mapigano hayo huku wengine wengi wakijeruhiwa.

0 comments:

Post a Comment