Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 20 October 2012

Maulamaa wa Russia wapinga marufuku ya hijabu

Baraza la Ulamaa  nchini Russia limepinga vikali  vitendo vya kibaguzi vinavyofanywa dhidi ya wanafunzi wanaovaa hijabu ya Kiislamu kwenye shule za nchi hiyo. Baraza la Ulamaa la Russia ni taasisi kubwa zaidi ya Kiislamu nchini humo, imeeleza kukerwa na kulaani vitendo vya unyanyasaji  dhidi ya wanafunzi wanaovaa hijabu ya Kiislamu kwenye shule za eneo la Stavropol nchini humo. Taarifa ya baraza hilo imeeleza kuwa, Waislamu kwa karne kadhaa sasa wamekuwa wakiishi kwa amani na upendo na wafuasi wa dini nyingine nchini humo. Taarifa ya baraza hilo imeeleza kuwa, mwanamke wa Kiislamu anayo haki ya kuvaa hijabu au kitambaa cha kichwani na kupiga picha itakayotumika kwenye hati ya kusafiria au kitambulisho cha uraia nchini Russia. Baraza la Ulamaa nchini Russia limewataka walimu wakuu na walimu wengine kuwaeleza wanafunzi thamani za kimaadili na kuwasihi wasijitumbukize kwenye vitendo vichafu, na siyo kuwanyima haki zao za kuvaa hijabu.

0 comments:

Post a Comment