Sikiliza Live
Saturday, 20 October 2012
JK AREJEA NCHINI AKARIBISHWA NA MADAI YA WAISLAMU
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpokea jana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara alipowasili kutoka katika ziara rasmi ya siku nne nchini Oman,
Rais Kikwete akiwa ameongozana na viongozi mbali mbali wakiwemo mkuu wa majeshi mkuu wa jeshi la polisi nchini alweza kushuhudia makundi kwa makundi ya waislamu njiani akielekea Ikulu jijini Dar es salaam walio kuwa wameandamana kudai kuachiwa kwa shekh Ponda na wenzake wanao shikiliwa na jeshi la polisi hasa baada kumyimwa dhamana na pia waumini hao wakitaka kiongozi wa Uamsho ambae alitoweka siku ya Ijumaa huku lakini waumini hao wamekuwa wakilishutumu jeshi la Polisi visiwani Zanzibar,Hata hivyo kiongozi wa uamsho ameweza kupatikana usiku wa kuamkia leo baada viongozi wa juu wa kundi hilo kuipa serikali masaa 24 ambayo yalikuwa yakamilike leo saa 10 jioni,wakati kiongozi wa Uamsho Shekh Fari Haad akipatikana na Shekh Ponda Issa Ponda na waumni wengine zaidi ya 32 hawaja achiliwa na jeshi la Polisi mpaka hivi sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment