Sikiliza Live
Saturday, 20 October 2012
HATIMAE KIONGO WA UAMSHO APATIKANA
Kwenye ukurasa wa uamsho wamesema Kiongozi huyo amepatikana hai usiku wa kuamkia leo.kabla uamsho waliipa serikali masaa 26 hadi leo alasiri amiri wao awe amepatikana vinginevyo hali itakuwa mbaya.
Sheikh Farid Hadi Ahmed mmoja kati ya viongozi wa ngazi za juu wa UAMSHO visiwani Zanzibar nchini Tanzania ameachiliwa huru jana usiku, baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi la nchi hiyo kwa muda wa siku tatu. Taarifa kutoka Zanzibar zinasema kuwa, Sheikh Farid Hadi Ahmed amethibitisha mwenyewe wakati alipowaambia waandishi wa habari jana usiku kwamba, askari kadhaa wa jeshi la polisi ndiyo waliomkamata siku ya Jumatano usiku, na kumpeleka mahala asipopajua kwa mahojiano. Wakati jeshi la polisi likiendelea kumhoji kwa siri kiongozi huyo wa UAMSHO, Mussa Ali Mussa Kamishna wa Polisi Zanzibar aliviambia vyombo vya habari kuwa, jeshi hilo halifahamu mahali alipo kiongozi huyo, na kwamba litaendelea na zoezi la kumtafuta. Kutoonekana kwa Sheikh Farid Hadi kulipelekea kuibuka ghasia na vurugu mjini Zanzibar, na kusababisha askari mmoja wa jeshi la polisi kuuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana. Hapo jana baada ya mshuko wa sala ya Ijumaa, askari polisi walipambana na Waislamu wenye hasira katika maeneo ya Mji Mkongwe Town wakilalamikia kutoonekana kwa kiongozi wao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment