Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 4 July 2013

Mahakama kuu Zimbabwe kutoakhirisha uchaguzi

                       
Mahakama ya Katiba ya Zimbabwe imekataa ombi la serikali ya nchi hiyo la kubadilisha tarehe iliyoainishwa kwa ajili ya kufanyika uchaguzi wa rais na bunge. Serikali ya Harare ilikuwa imeitaka mahakama hiyo kuakhirisha tarehe ya uchaguzi.
Mei 31 Mahakama ya Katiba ya Zimbabwe ilitoa hukumu na kutangaza kwamba uchaguzi wa rais na bunge wa nchi hiyo unapaswa kufanyika kabla ya Julai 31 mwaka huu wa 2013. Suala hilo linapingwa na wapinzani wa Rais Robert Mugabe ambapo Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai anaona kuwa wanahitajia muda zaidi ili kutekelezwa marekebisho ya kimsingi nchini kabla ya uchaguzi. Uchaguzi wa Rais na Bunge jipya la Zimbabwe unatazamia kuhitimisha shughuli za serikali ya mseto na umoja wa kitaifa.

 

0 comments:

Post a Comment