Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limewataka wananchi wanaotembelea maonyesho ya
kimataifa ya biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kutembelea banda lao
ili kujifunza kazi mbalimbali wanazofanya.
Hali kadhalika, limewataka Watanzania kuweka uzalendo kwanza kwenye kila jambo
ili kuijenga Tanzania kwa ajili yao.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, aliyasema hayo jana wakati akizungumza
na NIPASHE kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere katika maonyesho hayo
yaliyojumuisha washiriki 1,341 kutoka nchi 32.
Alisema uzalendo ndiyo nyenzo pekee ya kulijenga Taifa na kutokukubali kutumiwa
na mamluki wa ndani na nje wanaolitazama Taifa kwa jicho la husda.
"Tunawakaribisha Watanzania kufika kwenye banda hili kujifunza mambo
mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwaona makomandoo na jinsi Jeshi lilivyo na
wataalam katika sekta zote ambao kipindi cha amani hutumika kufanya shughuli za
maendeleo kama afya na ujenzi wa madaraja," alisema Kanali Mgawe.
Alisema matarajio ya wananchi wengi wanaofika kwenye banda hilo ni kuona silaha
na zana mbalimbali zinazotumika wakati wa vita.
Kanali Mgawe aliongeza kuwa lengo la kushiriki maonyesho hayo ni kueleza kazi
za Jeshi na kubadili mtazamo hasi kwa wananchi wawaone ni raia wa kawaida.
0 comments:
Post a Comment