Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 27 June 2013

Zuma ana siri nzito ya Mandela

 
Rais Jacob Zuma anaaminika kuwa na siri nzito ya Rais wa zamani wa nchi hiyo, Nelson Mandela baada ya kufuta safari ya kwenda Maputo, Msumbiji alikokuwa akahudhurie mkutano wa marais wa nchi wanachama wa Ushirikiano wa Maendeleo wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Zuma alivunja safari hiyo baada ya kumtembelea Mandela hospitalini na kumwona afya yake ikiwa imedhoofika, huku akiendelea kusaidiwa kupumua kwa mashine.
Hatua ya Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kuahirisha safari yake ya Maputo, tayari kumeibua sintofahamu zaidi kuhusu hatima ya afya ya Mandela.
Msemaji wa Rais Zuma, Mac Maharaj alisema kuendelea kuzorota kwa afya ya Mandela ni sababu ya kufutwa kwa safari hiyo.
Hata hivyo, Maharaj akizungumza kwa simu na gazeti hili jana alikataa katakata kuzungumzia undani wa afya ya Mandela, akasema jukumu hilo ni la familia yake na kwamba Ikulu inasaidia tu katika masuala ya jumla yanayohusu afya ya kiongozi huyo.

Familia ya Mandela
Wakati familia ya aliyekuwa mpigania amani na ubaguzi nchini Afrika Kusini, Nelson Mandela wakipeleka mashine ya kuchimbia kaburi katika makaburi ya kifamilia yaliyopo eneo la Qunu, kwa mara ya kwanza, kiongozi huyo amefumbua macho na kurejewa na fahamu.
Taarifa iliyotolewa jana jioni na Ikulu ya Afrika Kusini inasema Rais Zuma alimtembelea Mandela hospitalini mapema jana ambako alipewa taarifa kwamba anaendelea vizuri. “Bado yuko mahututi lakini imara,” ilisema taarifa ya Ikulu na kuongeza:
“Ana nafuu zaidi leo kuliko nilivyomwona jana (juzi) usiku. Timu ya madaktari inaendelea kumtibu.”
Hata hivyo taarifa hiyo ilimnukuu Rais Zuma akilalamikia kile alichosema kuwa ni vyombo vya habari kutoheshimu faragha ya mgonjwa.

 

0 comments:

Post a Comment