Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 27 June 2013

Mursi: Mgogoro wa kisiasa utalemeza Misri





Rais Mohammad Mursi wa Misri ameonya kuwa mgogoro wa kisiasa umeigawa nchi hiyo na yamkini jambo hilo likailemaza nchi hiyo.
Akizungumza Jumatano usiku kwa njia ya moja kwa moja ya televisheni, Mursi ametoa wito kwa mirengo yote ya kisiasa nchini humo kufungamana na sheria na kuingia katika mazungumzo ili kutatua matatizo yanayoikabili nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika.
Katika hotuba yake, Mursi amekiri kuwa amefanya makosa katika mwaka wake wa kwanza wa urais na kusema kuwa kila mtu anapaswa kujifunza kutokana na makosa aliyofanya. Mursi pia aliahidi kuanzisha marekebisho muhimu na ya haraka katika taasisi za serikali. Hotuba ya Mursi ilikuja masaa machache tu baada ya mapigano baina ya wafuasi wake na wapinzani katika mji wa Mansura katika eneo la Nile Delta. Duru zinaarifu kuwa karibu watu watano waliuawa na wengine 237 kujeruhiwa katika machafuko hayo ya jana. Wapinzani nchini Misri wameitisha maandamano makubwa kote nchini humo Juni 30 ambapo wanataka kumlazimisha Rais Mursi ajiuzulu. Wanamlaumu kiongozi huyo kuwa amekengeuka mkondo wa mapinduzi yaliyomtimua madarakani dikteta Hosni Mubarak. Uamuzi wa Mursi wa kukata uhusiano na Syria na kuwaunga mkono magaidi nchini humo pia ni jambo ambalo limewakasirisha wananchi wa Misri.

0 comments:

Post a Comment