Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 27 June 2013

Jeshi la Wanamaji Iran kuendelea kulinda doria kimataifa





Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Iran Admeli Habibullah Sayyari amesisitiza azma ya Jamhuri ya Kiislamu kuendelea kulinda doria katika maji ya kimataifa ili kuzihakikishia usalama meli za kibiashara za Iran na za kigeni.
Akizungumza Jumatano ya jana, Sayyari alisema tangu mwaka 2008 hadi sasa Jeshi la Wanamaji la Iran limesindikiza meli 2,000 za kibiashara na za mafuta. Amesema wanamaji wa Iran wamekabiliana mara 150 na makundi ya maharamia na kuwatia mbaroni na kisha kuwakabidhi kwa vyombo vya mahakama. Admeli Sayyari amesema meli za kivita za Iran pia huitikia wito wa msaada kutoka kwa meli za kibiashara za kigeni.
Tangu mwaka 2008 manoari za kivita za Iran zimekuwa zikilinda doria katika Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi kwa lengo la kukabiliana na maharamia. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya bahari IMO limepongeza mafanikio ya Jeshi la Wanamaji la Iran katika kukabiliana na maharamia.

0 comments:

Post a Comment