Ripoti
kutoka Ufaransa zinasema kuwa, idadi ya vijana wasio na ajira imeongezeka mno
nchini humo. Ufaransa ambayo inapitia kipindi kibaya zaidi cha kuzorota uchumi
katika historia ya nchi hiyo, kama zilivyo nchi nyingine za Ulaya inakabiliwa
na wimbi kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana. Taasisi ya Taifa ya Takwimu ya
Ufaransa na Utafiti wa Kiuchumi imetoa ripoti yake mwezi huu wa Juni na
kubainisha kwamba, kiwango cha ukosefu wa ajira nchini humo kimefikia asilimia
10.8. Kwa mujibu wa taasisi hiyo ya takwimu, kiwango hicho ni kikubwa kabisa
kuwahi kushuhudiwa nchini Ufaransa katika kipindi cha miaka 14 iliyopita.
Taarifa zaidi zinasema, hali ya ukosefu wa ajira kwa vijana ni mbaya zaidi
ikilinganishwa na matabaka mengine ya jamii kwani mmoja kati ya kila vijana
wanne wa Kifaransa, hana kazi na wala uwezo wa kuwa na chanzo cha kumpatia
kipato. Kwa mujibu wa takwimu rasmi, takribani vijana milioni moja na laki tisa
wenye umri kati ya miaka 15 hadi 29 nchini Ufaransa hawana kazi, hawasomi na
wala hawajishughulishi na kozi au ufundi wa aina yoyote. Huku hayo yakiripotiwa
kiwango cha vijana wasio na ajira katika Umoja wa Ulaya kilifikia milioni 24.4
mwezi Aprili mwaka huu.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment