Bunge la Sudan limesisitiza juu ya ulazima wa kuungwa mkono jeshi la 
nchi hiyo katika kuwaangamiza waasi katika maeneo mbalimbali nchini 
humo. Mehdi Ibrahim Mkuu wa Mrengo wa 'Kongresi ya Taifa' katika bunge 
la Sudan amesema kuwa, uungaji mkono kwa jeshi la nchi hiyo katika 
kuwasambaratisha waasi, ni jukumu la kitaifa. Ameongeza kuwa, operesheni
 za kuyakomboa maeneo yaliyokuwa yakidhibitiwa na makundi ya waasi 
katika jimbo la Kordofan Kusini zinapasa kuendelea na kuwataka wananchi 
waliunge mkono jeshi la nchi hiyo. Mbunge huyo kutoka mrengo wa Kongresi
 ya Taifa amesisitiza juu ya kuongezwa bajeti ya jeshi, kwa lengo la 
kununua zana na silaha za kisasa na kuboresha hali ya kimaisha ya 
wanajeshi wa nchi hiyo. Serikali ya Sudan imekuwa ikizituhumu nchi za 
Sudan Kusini, Uganda na utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa zinayaunga 
mkono makundi ya waasi katika maeneo ya kusini na magharibi mwa Sudan.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 comments:
Post a Comment