Zaidi ya watu 100 wameuawa katika machafuko ya siku mbili 
yaliyotokea nchini Iraq baada ya kujiri mapigano kati ya askari jeshi na
 waandamanaji na pia watu wenye silaha katika mji wa Kirkuk kaskazini 
mwa nchi hiyo. Machafuko hayo yalianza baada ya waandamanaji kwenye mji 
wa al Hawijah kuzusha fujo eti wakidai damu ya dikteta wa zamani wa nchi
 hiyo Saddam Hussein. Serikali ya Iraq inasema kuwa, vujo na machafuko 
hayo yanasababishwa na mtandao wa al Qaida na wafuasi wa chama cha Baath
 kilichoondolewa madarakani.
Kwingineko watu 15 wameuawa na wengine 42 kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokea kati ya vikosi vya jeshi la Iraq na wanamgambo wenye silaha kwenye mkoa wa Salahuddin ambapo wanamgambo hao walivamia vituo kadhaa vya upekuzi.
   
0 comments:
Post a Comment