Khalid Mash'al Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano
ya Kiislamu ya Palestina Hamas jana usiku alipitishwa na wajumbe wa
ngazi za juu wa harakati hiyo kuendelea kushikilia wadhifa wake huo kwa
kipindi cha miaka minne ijayo.
Taarifa kutoka Cairo zinasema kuwa, Ismail Haniya, Waziri Mkuu wa serikali halali iliyochaguliwa na wananchi wa Palestina ambaye hivi sasa yuko nchini Misri pamoja na Mussa Abu Marzouq watakuwa wasaidizi wa Khalid Mash al. Hali kadhalika viongozi waandamizi wa Hamas waliwachagua wajumbe wa kamati ya utendaji wa chama hicho. Awali, Khalid Mash'al alitangaza kuwa atang'atuka kwenye wadhifa huo utakapomalizika muda wa uongozi wake, lakini viongozi waandamizi wa Hamas wamepinga mpango huo na kumtaka aendelee kushikilia wadhifa huo.

0 comments:
Post a Comment