Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 6 November 2012

Somalia yaanza kukusanya silaha zisizo na vibali

Serikali ya Somalia imeanza kukusanya silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.
Kiongozi mmoja mwandamizi wa jeshi la Somalia amesema kuwa, zoezi hilo endelevu limeanzishwa kutokana na amri iliyotolewa na serikali ya nchi hiyo. Amesema kuwa, raia na wafanyakazi wa serikali wanaomiliki silaha kinyume cha sheria wanapaswa kuzikabidhi.
Zoezi hilo limefanyika bila ya kutolewa taarifa za awali ili kuhakikisha amani inarejea katika mjikuu Mogadishu. Wananchi wa Somalia na hasa katika mji mkuu wa nchi hiyo walikuwa wakitembea na silaha kinyume cha sheria wakihofia kutokea mapigano wakati wowote ule.
Viongozi wengi wa serikali, wafanyabiashara na shakhsia mashuhuri mjini Mogadishu walikuwa wakiwatumia walinzi binafsi kutoka makabila na koo zao kutokana na ukosefu wa polisi imara na  jeshi lenye nguvu nchini Somalia.

0 comments:

Post a Comment