Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 6 November 2012

Misri yataka kukaguliwa silaha za nyuklia za Israel

Serikali ya Misri imeutaka Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA ukagua mitambo ya silaha za nyuklia ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Amr Roushdy Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Misri amesema kuwa, ujumbe wa Cairo kwenye Umoja wa Mataifa umeutaka wakala wa IAEA kukagua mitambo ya silaha za nyuklia ya utawala wa Israel. Roushdy ameongeza kuwa, Mootaz Ahmadein Khalil, Balozi wa Kudumu wa Misri kwenye Umoja wa Mataifa ametoa taarifa hiyo mbele ya kikao cha Baraza Kuu la umoja huo na kuongeza kwamba, utawala ghasibu wa Israel unapuuza maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Mootaz Ahmadein Khalil amesema kwamba, utawala ghasibu wa Israel  pekee ndio unaozakisha silaha za  nyuklia  katika eneo la Mashariki ya Kati, jambo ambalo ni hatari na yumkini likazidisha silaha za nyuklia katika eneo hili na hatimaye kukwamisha mpango wa kulifanya eneo hili kutokuwa na silaha za nyuklia.

0 comments:

Post a Comment