Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday 9 June 2013

Wasimamizi laki mbili kusimamia uchaguzi Iran

                               

 
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema maafisa laki mbili watasimamia uchaguzi kote nchini huku elfu sita kati yao wakiwa katika vituo vya kupigia kura mjini Tehran.
Akizungumza na waandishi habari mjini Tehran, Waziri wa Mambo ya Ndani Mostafa Mohammad-Najjar amesema wizara yake ina nafasi muhimu katika kusimamia uchaguzi. Huku zikiwa zimebakia siku chache kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na vile vile wa mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji, wizara ya mambo ya ndani imebainisha sheria zitakazofuatwa katika uchaguzi. Najjar amesema Wairani zaidi ya milioni 50 wametimiza masharti ya kupiga kura na kwamba Wairani wanaoishi nje ya nchi pia watapata fursa ya kupiga kura katika uchaguzi wa rais. Uchaguzi wa rais wa awamu ya 11 utafanyika Juni 14 na mshindi wa uchaguzi huo atachukua nafasi ya Rais Mahmoud Ahmadinejad anayemaliza muda wake na ambaye kwa mujibu wa katiba hawezi kugombea mara hii baada ya kuhudumu kwa mihula miwili mfululizo. Kuna wagombea wanane wa kiti cha urais ambao ni pamoja Saeed Jalili,   Ghulam Ali Haddad Adel, Mohsen Rezai, Sheikh Hassan Rohani, Mohammad-Reza Aref, Mohammad Gharazi, Mohammad Bager Qalibaf na Ali Akbar Velayati.

0 comments:

Post a Comment