Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 18 June 2013

`Wafichueni viongozi wazembe`

Chama cha Mapinduzi CCM kimewataka wananchi kuwafichua na kuwataja viongozi na watendaji wabovu ili waweze kushughulikiwa kabla hawajawa kero.Wito huo ulitolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho wilaya ya Tanga, Kassim Kisauji, wakati akizindua Chuo cha Biashara cha Masuguru kilichopo mjini Muheza.
Kisauji ambaye ni Meya Mstaafu wa Jiji la Tanga, aliwataka wananchi kutowafumbia macho watendaji wabovu na badala yake watoe taarifa zao kwa viongozi ili waweze kuchukuliwa hatua.
 
“Wananchi msisubiri matatizo yakaendeleo kuwa kero, mbona madaraka sasa yameletwa kwenu huku chini, tatizo liko wapi?...elezeni kwa wakubwa watu ambao ni kikwazo wawajibishwe” alisema Kisauji.
 
Aliwataka wananchi kuacha kuwafumbia macho watendaji wabovu kwani wao ndiyo wahanga na kwamba watu hao pia wanakichafua Chama cha Mapinduzi kwa kuonekana kimeshindwa kufanyakazi.
 
 Kwa upande mwingine, Kisauji alisema kuwa lengo la serikali ni kuwawezesha wafanyabiashara wenye mikakati ya kuwekeza kwa kuandaa mazingira mazuri yakuwafanya watoe huduma bora kwa wananchi.
 
Mkurugenzi wa Mtandao wa Wanawake wa Inuka unaosimamia chuo hicho, David Msuya, alieleza kuwa jumla ya wanafunzi 30 wamejiunga tangu kuanzishwa kwake mapema mwaka huu.
 
Alitaja kozi 14 zinazotolewa chuoni hapo kuwa ni, utunzaji kumbukumbu na nyaraka za serikali, hoteli, uhasibu, ujasiliamali, ufundi cherahani, uongozi,  utawala na ualimu wa chekechea. 
 
Kozi nyingine ni uandishi wa habari, sheria za michezo, uongozi wa watalii, mawasiliano kwa umma, kozi za bandari, ukatibu muhtasi na ukusanyaji wa mapato.
 

0 comments:

Post a Comment