Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 18 June 2013

Vikwazo haviathiri miradi ya nyuklia ya Iran

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA amesema kuwa, licha ya kuongezwa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran, lakini miradi ya nyuklia ya Iran inayofanyika kwa amani inazidi kuendelea na vikwazo hivyo havina athari yoyote kwa nchi hiyo. Yukiya Amano amesema kuwa, wakala wa IAEA una azma ya kuendeleza duru nyingine ya mazungumzo ya nyuklia na Iran, ingawa tarehe ya kufanyika mazungumzo hayo haijaainishwa.
Matamshi ya Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa IAEA yanatolewa katika hali ambayo, Dakta Hassan Ruhani Rais Mteule wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliwaambia waandishi wa habari hapo jana kuwa, serikali yake itahakikisha kuwa kuna uwazi katika mipango hiyo ya nyuklia ili kuuthibitisia ulimwengu kwamba Iran ya Kiislamu haina nia ya kuunda bomu la atomiki, bali miradi hiyo inafanyika kwa malengo ya amani.

0 comments:

Post a Comment