Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 18 June 2013

UN yaingiwa wasiwasi na amani nchini Kongo
Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameelezea wasiwasi wa hali ya usalama na amani kusini mwa nchi hiyo.
Roger Meece amesema kuwa, machafuko yaliyotokea katika jimbo tajiri kwa madini  na maliasili la Katanga, ni jambo lenye kutia wasiwasi mkubwa. Roger Allen Meece amesisitiza kuwa, kuna ulazima wa kukomeshwa machafuko kwenye jimbo hilo kwa kutumia njia za kisiasa na mazungumzo.
Mjumbe maalumu wa Ban Ki moon ameongeza kuwa, hatua ya kupelekwa wanajeshi zaidi katika jimbo la Katanga itasababisha machafuko zaidi katika eneo hilo.
Wakaazi wa maeneo mashariki  mwa Kongo wanakosoa vikali utendaji wa vikosi vya Umoja wa Mataifa vilivyoko katika eneo hilo kwa kushindwa kufanya juhudi zozote za kuleta amani.


0 comments:

Post a Comment