Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 11 June 2013

Uasi waongezeka nchini Chad na Niger

                                        03 Shaaban,1434 Hijiriyah/ June12 ,2013 Miyladiyah
 Katika hali ambayo, Ufaransa bado inashindwa kutangaza ushindi dhidi ya waasi huko nchini Mali, vyombo vya habari vimeripoti kuanza harakati mpya za uasi katika nchi mbili za Chad na Niger. Ripoti zaidi zinaeleza kuwa, kuna uwezekano mkubwa wanamgambo wa Mali waliokimbilia huko kusini mwa Libya baada ya mashambulizi ya askari wa Ufaransa na Mali dhidi ya maeneo yao ya kaskazini mwa Mali, nao wakaanzisha mashambulizi mapya dhidi ya nchi za Chad na Niger na kwamba, viongozi wa nchi hizo hawana tena utulivu wa moyo kama hapo kabla. Mwanadiplomasia mmoja wa Niger amenukuliwa akisema kuwa, hadi hivi sasa hali ya mambo haitabiriki na kwamba, nchi hizo mbili zinaishi kwa wasiwasi mkubwa huku zikiweka mipango madhubuti ya kuimarisha ulinzi na usalama. Kwa upande wake, Mathieu Pellerin mtafiti katika Shirika la Mahusiano la Kimataifa la nchini Ufaransa amethibitisha kuwepo makundi ya wanamgambo huko kusini mwa Libya na kusisitiza kuwa, wanamgambo hao wamejizatiti kwa silaha nzito tangu kipindi cha utawala wa Kanal Muammar Gaddafi sambamba na kuanzisha kambi za mafunzo ya kijeshi katika eneo hilo.

0 comments:

Post a Comment