Mabadiliko katika orodha ya mambo ya Muungano yamekuwa yakifanyika kwa kuzingatia Katiba na sheria kwa madhumuni ya kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Aboud, wakati akijibu swali la Mwakilishi Saleh Nassor Juma wa Jimbo la Wawi katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea, Chukwani Zanzibar.
Alisema ipo hati ya makubadiliano kuhusu mambo ya muungano na
marekebisho yake yamekuwa yakifanyika kwa ridhaa ya Bunge kama chombo
cha wawakilishi wa wananchi wa pande mbili za muungano.
“Mheshimiwa Spika mabadiliko yote yaliofanyika katika orodha ya
mambo ya muungano yamefanyika kihalali kwa kuzingatia Katiba na sheria
kwa madhumuni ya kuimarisha muungano wenyewe.” alisema Waziri Aboud.
Hata hivyo, alisema tangu kufikiwa kwa Muungano mwaka 1964,
Zanzibar imetoa nafasi ya Waziri Mkuu mara moja pamoja na Mwenyekiti wa
Bunge mwaka 2005 hadi 2010.
Alisema wadhifa wa Waziri Mkuu umewahi kushikwa na Mzanzibari,
Salim Ahmed Salim, sawa na wadhifa wa Mwenyekiti wa Bunge, Zuberi Ali
Maulid, ambao walionyesha uwezo mkubwa katika kutumikia Taifa.
“Mheshimiwa Spika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hadi
sasa ndiyo inayotuongoza haikusema vigezo vya uteuzi wa Waziri Mkuu bali
imetoa mamlaka ya uteuzi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,”
alisema Waziri Aboud.
Hata hivyo, aliwaeleeza Wawakilishi kuwa Zanzibar haijawahi kutoa
nafasi ya Spika wa Bunge wala Naibu wake, lakini wabunge kutoka Zanzibar
na Tanzania wote wanahaki sawa kugombea nafasi hiyo.
Waziri Aboud alisema kwamba serikali imeamua kuanzisha mchakato wa
mabadiliko ya Katiba ya Muungano kwa malengo ya kuondoa kero za muungano
na kuwataka wananchi kupitia mabaraza ya katiba na Bunge kutumia nafasi
hiyo ili kufanikisha kupata katiba mpya.
0 comments:
Post a Comment