Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 27 June 2013

Nzige wavamia Madagascar





Nchini Madagascar baa la nzige ambalo udhibiti wake unatia mashaka linaripotiwa kutishia usalama na uhakika wa chakula nchini humo.
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula Duniani (FAO), ifikapo mwezi Septemba mwaka huu karibu theluthi moja ya Madagascar itakuwa imevamiwa na nzige na kuyaweka kwenye hatari karibu maisha ya watu milioni 13 au karibu asilimia 60 ya watu wote wa nchi hiyo.
FAO imefanya hitihada za kuchangisha dola milioni 22 kugharamia hatua za dharura za kukabiliana na nzige lakini kampeni hiyo haijaungwa mkono kikamilifu ikiwa inakabiliwa na uhaba wa fedha. Mkurugenzi wa FAO Jose Graziano da Solva anasema kuwa iwapo nzige hao hawatadhibitiwa huenda athari zao zikawa za miaka mingi na pia watakuwa vigumu kuwazuia tena kwa gharama kubwa.

0 comments:

Post a Comment