Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 13 June 2013

Mfumo mpya wa usambazaji pembejeo wabuniwa Serikali imebuni mfumo mpya wa usambazaji wa pembejeo utakaotumika katika msimu wa kilimo wa 2013/14.

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima aliliambia Bunge mjini hapa jana kuwa, mfumo huo umejadiliwa katika semina ya usambazaji wa pembejeo iliyofanyika Mei mwaka huu.

Kuhusu kuchelewa kwa pembejeo, alisema upatikanaji wa pembejeo nchini unahusisha pembejeo zinazotolewa kwa  ruzuku na serikali na pembejeo zinazouzwa na wafanyabiashara kwa utaratibu wa soko.

Malima alisema pembejeo yenye ruzuku inaagizwa na kusambazwa kwa utaratibu maalum na kampuni na mawakala walioteuliwa ili kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo hizo kwa bei iliyopangwa na serikali wanapata unafuu wa bei kupitia ruzuku.

0 comments:

Post a Comment