Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday 9 June 2013

MAKAMBA: DHAMIRA ya mfumo wa vyama vingi BADO HAIJAFIKIWA

                               

 NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba amesema dhamira ya kuwepo kwa vyama vingi bado haijafikiwa tangu kuanzishwa kwake kutokana na kukosa vyama na viongozi  wenye dira kwa Taifa.
 Aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wamnafunzi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ambao wanamaliza vyuo mbalimbali mkoa wa Dar es Salaam.
 Makamba ambaye pia ni Mlezi wa Vyuo Vikuu Tanzania alisema  vyama hivyo vimekuwa vikijikita katika kulalamika bila kuonyesha dira na mwelekeo tofauti jambo ambalo linapelekea katika kufanya fujo ambazo zinakwamisha jitihada za serikali.
 Makamba alisema Serikali inafanya kazi kutokana na mipango yake ambayo imejiwekea yenyewe hivyo inaamini kuwa itafikia malengo yake bila kusukumwa na mtu.
 “Kwa  kweli najuta kwanini tuliruhusu uwepo wa vyama vingi hapa nchini kwani lengo letu lilikuwa ni kudumisha demokrasia kitu ambacho kimekuwa kinyume kwani vyama na  viongozi hao wamekuwa wakihubiri kinyume na dhima ya lengo husika,” alisema
 Naibu Waziri alisema CCM ni chama ambacho kinaheshimika kitaifa na kimataifa hivyo wao wanaamini kuwa heshima hiyo itaendelea kuwepo milele kwa milele.
Alisema vijana wa CCM wahakikishe kuwa wanakisaidia chama na  nchi kwa ujumla ili nchi isije kuchukuliwa na vyama vya upinzani kwani itakuwa ni sawa na kuipeleka nchi kuzimu.
 Aidha Mlezi huyo aliwataka vijana  hao wanaomaliza kujiamini na kuthubutu kushiriki katika fursa mbalimbali zinazojitokeza ili waweze kupata urahisi wa kushiriki katika chama na serikali kwani ni wajibu wao kulitumikia Taifa.
Makamba alisema vijana wanapaswa kushiriki katika harakati za kisiasa kwani hayupo mtu amnbaye atapata jambo bila kulihitaji mwenyewe na kuondokana na dhana ya kutafutiwa kazi kama wengi wanaofikiri.
 Aliwataka wingi wao uwe ni sehemu muhimu ya kutafakari muafaka wa Taifa la Tanzania ijao ikiwa ni kushiriki katika ngazi mbalimbali za uongozi na kuondokana na dhana kuwa mwenye uwezo wa fedha ndio sababu ya kushinda.
Mlezi huyo alisema dhana ya fedha katika kutafuta uongozi  ipo kwa baadhi ya watu kutokana na tabia ya mtu mmoja mmoja lakini sio jambo la kusimamia kama kigezo.
 Naibu Waziri aliwataka vijana wa CCM kuondoa uoga katika maamuzi ambayo yanahusu maslahi ya Taifa na jamii kwa ujumla iwapo sifa za uongozi unazo.
Makamba aliwaambia vijana kutambua kuwa kiongozi wema wanatoka kwa mungu na kuachana na tabia ya kulalamika kwakigezo kuwa nchi inaongozwa na wazee jambo ambalo wanalitengeneza wenyewe.
 Aidha aliwataka wasomi kutafuta maandiko ambayo aliandika Hayati Mwalimu Nyerere kwani yana msingi mkubwa katika kujitambua na kufanya maamuzi sahihi kuhusu nchi yao na uongozi kwa ujumla.
 Naye Mwenyekiti  Vyuo Vikuu Wilaya ya Dar es Salaam Abubakari Asenga alisema katika mahafal;i hayo wanafunzi zaidi ya mmia nne kutoka vyuo 28 vya mkoa wa Dar es Salaam walishiriki katika sherehe hiyo.
 Asenga alisema huo ni uataratibu ambao wamekuwa nao tangu kuoanzishwa kwa shirikisho hilo lengo likiwa ni kuwatambua na kuwapatia vyeti vya utambulisho wao ndani ya CCM.
 Alitaja vyuo ambavyo vilishiriki ni pamoja na Mwalimu Nyerere, Ustawi, Ardhi, UDSM, IFM, CBE, DIT, TSJ na vingine vingi.
 Kwa upande wa msoma risala kwa niaba ya wahitimu Innocent Nsena  alisema wanakiomba Chama Cha Mapinduzi CCM kuwatumia wahitimu wanaomaliza vyuo kwani wana ujuzi na uwezo wa kukabiliana na  changamoto za jamii pamoja na vyama vya upinzani hapa nchini.
 Aidha alisema wanavyuo wanapendekeza maoni yao kuhusu rasimu ya katiba ambapo wanaomba nchi ya Tanzania kutokubali kuwa na serikali ya shirikisho kwani uwezo wa nchi bado ni mdogo kuendesha nchi ambayo bado ni change kuichumi.
 Pia wanapendekeza upatikanaji mpya wa kupata mgombea urais ili kuondoa mpasuko ambao unatokea mara kwa mara baada ya uchaguzi kufanyika.
Alisema katika mazingira yoyote yale Rais bora lazima atokee CCM ila kutokana na mazingira mbalimbali ambayo yamekuwa yakitokea baada ya uchaguzi ni vyema wakatumia mfumo wa kujaza dodoso ili wana CCM wapendekeze Rais wanayemuhitaji kwa manufaa ya Taifa.

0 comments:

Post a Comment