Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 18 June 2013

Libya kusikiliza kesi ya mtoto wa Gaddafi Mahakama ya Libya imetangaza kuwa kesi inayowakabili Seiful Islam Gaddafi mtoto  wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi na Abdullah Sanusi Mkuu wa zamani wa shirika la Kiintelijinsia la nchi hiyo itasikilizwa mwezi Agosti mwaka huu nchini humo. Serikali ya Libya imekataa kuwakabidhi watuhumiwa hao wa mauaji ya wananchi wa nchi hiyo wakati wa utawala wa Gaddafi kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC iliyoko nchini Uholanzi. Hatua ya Libya ya kutaka watuhumiwa hao wahukumiwe nchini humo imezua mivutano mikubwa na mahakama ya ICC kwani mahakama hiyo ya kimataifa inadai kwamba, mazingira yaliyopo hivi sasa nchini Libya hayawezi kuendesha kesi za watuhumiwa hao.

0 comments:

Post a Comment