Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 11 June 2013

Kuongezeka ubaguzi dhidi ya Waislamu Uingereza

                           03 Shaaban,1434 Hijiriyah/ June12 ,2013 Miyladiyah
 Jengo la Waislamu la Somali Bravanese Welfare Association lililoteketezwa moto London wiki iliyopita.

 Imeelezwa kuwa vitendo na miamala mibaya dhidi ya jamii ya Waislamu nchini Uingereza vimeongezeka maradufu katika siku za hivi karibuni baada ya kuuawa askari mmoja wa Uingereza, huko kusini mashariki mwa London. Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi mjini London Simon Latchford na kuongeza kuwa, vitendo vya kibaguzi dhidi ya Waislamu, vimeongezeka kwa asilimia nane. Amesema vitendo hivyo vimeongezeka katika hali ambayo awali vilikuwa sawa na asilimia moja tu. Aidha afisa huyo wa polisi mjini London amekiri kuwa, baadhi ya vitendo kama hivyo haviripotiwi kwa polisi na wala kwa vyombo vya habari nchini humo. Hii ni katika hali ambayo, baada ya kuchomwa moto shule moja ya Waislamu huko kusini mwa mji mkuu wa Uingereza, London, polisi ilitangaza kuzidisha doria katika maeneo tofauti ya mji huo ili kuilinda jamii Waislamu mjini humo. Mauaji ya askari Lee Rigby yaliyotokea katika eneo la Woolwich, kusini mashariki mwa London, yanatajwa kuwa chanzo cha kuongezeka ubaguzi dhidi ya jamii ya Waislamu nchini Uingereza.

0 comments:

Post a Comment