Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday, 16 June 2013

Kuanzishwa Mfuko wa Maendeleo ya Komoro

                             

 Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ' Arab League' umeamua kuanzisha Mfuko wa Maendeleo na Uwekezaji nchini  Komoro utakaokuwa na thamani ya dola milioni mia tano. Sheikh Ahmad bin Muhammad Aal Thani Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Qatar anayehusika na mashirikiano ya kimataifa na ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maendeleo na uwekezaji wa jumuiya hiyo nchini Komoro amesema kuwa, mfuko huo umeanzishwa kwa lengo la kuunga mkono na kutekelezwa miradi ya kimaendeleo na ya uwekezaji visiwani humo. Amesema kuwa, lengo kuu la kuanzishwa mfuko huo ni kuinasua nchi hiyo na lindi la umasikini. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Visiwa vya Komoro licha ya kuwa ni mwanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu 'Arab League' ni mwanachama pia wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC.

0 comments:

Post a Comment