Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 13 June 2013

Jackob Zuma: Mandela anaendelea vizuri

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema kuwa, Nelson Mandela rais wa kwanza wa nchi hiyo baada ya kusambaratika utawala wa ubaguzi wa rangi anaendelea vizuri na matibabu, baada ya kuzidiwa siku kadhaa zilizopita.
Akihutubia bungeni jana, Zuma alisema, wana furaha kuona maendeleo mazuri ya afya ya Mandela na kwamba wanaomba wananchi wote wa Afrika Kusini na jamii ya kimataifa kuendelea kumuombea Mzee Mandela ili apone haraka.
Kiongozi huyo mkongwe wa kupinga ubaguzi wa rangi barani Afrika, siku ya Jumamosi alikimbizwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya kutokana na matatizo ya mapafu.
Mzee Mandela mwenye umri wa miaka 94 amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara katika siku za hivi karibuni

0 comments:

Post a Comment