Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 11 June 2013

Iran yalaani ujasusi wa Marekani katika intaneti

                                 03 Shaaban,1434 Hijiriyah/ June12 ,2013 Miyladiyah
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali mradi mkubwa wa serikali ya Marekani wa kuwafanyia ujasusi watumiaji wa Intaneti duniani. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Sayyid Abbas Araqchi akizungumza na waandishi habari Tehran Jumanne hii amesema, ujasusi wa Marekani katika mitandao ya Intaneti 'si jambo jipya' na kuongeza kuwa ujasusi huo unakiuka misingi ya demokrasia ambayo Marekani inadai kuitetea.
Hivi karibuni gazeti la The Guardian la Uingereza lilifichua namna Shirika la Usalama wa Taifa Marekani NSA linavyochukua habari za kijasusi kutoka kwa mabilioni ya watumiaji wa Intaneti duniani.
Kuhusiana na kadhia ya Syria, Araqchi amesema, Iran inaunga mkono juhudi za Russia za kuandaa kongamano huko Geneva kwa lengo la kuutatua mgogoro wa Syria kwa njia ya mazungumzo. Amesema kikao hicho kitafanikiwa iwapo kitazishirikisha nchi zote ambazo zinaweza kuwa na nafasi ya kusaidia utatuzi wa mgogoro wa Syria. Kuhusiana na uchaguzi ujao wa rais wa Iran, Araqchi amesema, Wairani waishio katika nchi 96 duniani watapata fursa ya kupiga kura katika ofisi 128 za kibalozi za Iran. Aidha ametoa wito kwa nchi zote hasa za Ulaya kulinda vituo vya kupigia kura vya Iran na kutoruhusu makundi ya kigaidi kuvurga zoezi hilo la uchaguzi.

0 comments:

Post a Comment