Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday 9 June 2013

Ghasia za Mtwara TZ, mbunge atiwa mbaroni

                                  

 
Polisi nchini Tanzania wamemkamata mbunge wa Mtwara Mjini Hasnain Murji kwa tuhuma za kuchochea vurugu za kupinga mradi wa bomba la gesi kutoka mkoani humo kwenda mji mkuu wa nchi hiyo Dar es Salaam.
Msemaji wa Jeshi la polisi nchini Tanzania, Advera Senso amenukuliwa na vyombo vya habari nchini Tanzania akisema kuwa Murji ambaye ni mbunge wa chama tawala CCM alikamatwa nyumbani kwake maeneo ya Shangani mjini Mtwara. Hivi karibuni pia viongozi wanne wa vyama vya upinzani mkoani Mtwara walikamatwa na kufikishwa katika mahakama ya Mtwara Juni 4, wakikabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama, kufanya uchochezi na kuamsha hisia mbaya miongoni mwa Watanzania.
Murji amekamatwa ikiwa zimepita zaidi ya wiki mbili tangu kutokea vurugu kubwa mkoani Mtwara. Ghasia hizo katika mkoa huo wa kusini magharibi mwa Tanzania zilidumu kwa siku mbili, ambapo polisi walipambana na makundi ya vijana wanaopinga mradi wa bomba la gesi kujengwa. Watu kadhaa walipoteza maisha katika vurugu hizo na mali nyingi kuharibiwa. Wakaazi wa Mtwara wanapinga wazo la kusafirishwa gesi nje ya eneo hilo kwa njia ya bomba. Wanasema gesi inapaswa kusafishwa katika eneo hilo kabla ya kusafirishwa ili wenyeji wapate ajira.

0 comments:

Post a Comment