Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 11 June 2013

'Fidia ya Uingereza kwa Mau Mau Kenya haitoshi'

                        03 Shaaban,1434 Hijiriyah/ June12 ,2013 Miyladiyah
 Askari wa kikoloni wa Uingereza wakiwa wamewashikilia wapiganaji wa Mau Mau mwaka 1952.Mbunge maarufu wa Uingereza, George Galloway wa Chama cha Respect amelaani vikali fidia ndogo sana iliyotolewa na serikali ya London kwa Wakenya ambao waliteswa na haki zao kuvunjwa wakati wa utawala wa kikoloni wa Uingereza nchini Kenya kwenye muongo wa 50.
Akizungumza katika kipindi chake cha kila wiki cha 'Comment' katika kanali ya televisheni ya Press TV, Galloway amesema, Paundi Milioni 20 zinaonekana nyingi lakini kila mhanga atapata paundi elfu tatu tu au shilingi laki nne za Kenya.
Galloway amejadili namna Wakenya wa harakati ya Mau Mau walivyopigania ukombozi kutoka ukoloni wa Uingereza na kusema, fidia wanayolipwa si chochote si lolote ikilinganishwa na namna walivyoteswa na vikosi vya kikoloni. Amesema wanaume walihasiwa, wanawake walinajisiwa mara kadhaa mbali na mateso mengine ya kinyama na kwa hivyo fidia hiyo haitoshi hata kidogo. Uingereza imetoa fidia kwa Wakenya 5,228 pekee katika hali ambayo Kamisheni ya Haki za Binadamu nchini Kenya inasema kuwa zaidi ya Wakenya 90,000 waliteswa au kuuliwa na wakoloni wa Uingereza katika muongo wa 50. Aidha watu 160,000 waliwekwa kizuizini katika mazingira ya kuogofya. Galloway pia amesema, bado kuna mamia ya maelfu ya wahanga wa jinai za Uingereza ambao hawajalipwa fidia kote duniani.

0 comments:

Post a Comment